Headlines News :
KARIBU ZANZIBAR YETU BLOG, KWA HABARI MOTO MOTO KUTOKA JIKONI USIKOSE KUTUFUATILIA...ZANZIBAR MEDIA GROUP TUNAIWAKILISHA ZANZIBAR...
Home » » WATOTO 30,000 KUPATIWA CHANJO

WATOTO 30,000 KUPATIWA CHANJO




ZAIDI ya watoto 30,000 wenye umri wa miezi 6 hadi miaka 5 wa wilaya ya Magharibi ‘A’ na ‘B’ wanatarajiwa kupewa chanjo za vitamin ‘A’ na dawa za minyoo kwa kipindi cha mwezi mmoja ili kuwakinga na maradhi mbalimbali katika kipindi cha ukuaji wao.

Akizindua utoaji wa chanjo kwa watoto katika kituo cha afya Magogoni, Mkurugenzi wa Manispaa Magharibi ‘B’ Amour Ali, amesema watoto chini ya umri wa miaka mitano wamekuwa wakiathirika na kupata maradhi ikiwemo shrua, pepopunda, kuharisha na kupooza kutoka na ukosefu wa chanjo.

Alifahamisha kuwa chanjo zina umuhimu mkubwa kwa watoto kwani husaidia katika makuaji yao iwapo watapata lishe pamoja na matone ya vitamin A hali itakayosaidia kustawisha afya zao.

Daktari dhamana wilaya ya Magharibi, Dk. Rahma Maisara, na Mtaalamu wa afya na lishe kutoka UNICEF,  Shemsa Mselem, walisema watoto walio chini ya umri wa miaka mitano wamekua wakipoteza maisha kutokana na ukosefu wa chanjo kutokana na upungufu wa damu unaosababishwa na ukosefu wa vitamin.

Nao wananchi waliopatiwa huduma hiyo waliunga mkono jitihada za serikali za kuwapatia chanjo watoto kwani zinasaidia kuwakinga na maradhi watoto wao jambo ambalo hapo awali halikuwepo.
Share this article :

No comments:

Post a Comment

 
Support : Zanzibar Media Group
Copyright © 2020. Zanzibar Yetu - All Rights Reserved