Jawabu kutoka kwa Sheikh Shaaban Bin Salim Al-Battashi
Muisilaamu baada ya
kufa kwake, anatakiwa kufanyiwa haki zake maalumu kisheria.
Na miongini mwa haki zake ni :
Kulipwa madeni yake kutokana na asili ya mali yake
Kukafiniwa sanda
Kusaliwa
Kuzikwa
Kuombewa dua
Katika kuombewa dua
hakuna muda maalumu ambao umewekwa kisheria kuwa ndio muda wa kumuombea maiti
Wala hakuna Sunna
yoyote ya kukusanyika watu na kumuombea dua maiti
Mtume S.A.W alikuwa
akiwaambia maswahaba r.a baada ya kuzika
maneno yafuatayo
"Muombeeni msamaha ndugu yenu, kwa hakika yeye hivi sasa ataulizwa"
Amma kukusanyika watu
siku ya tatu, au arobaini, au mmwezi wa Rajabu, kwa ajili ya kuwaombea dua
maiti, hili jambo halipo hatika sunna ya Mtume s.a.w, wala yoyote katika maswahaba R.A
Bali hili jambo ni uzushi katika dini
Na wala hakuna thawabu kwa mwenye kualika watu kufanya matanga katika msiba, na mwenye kula chakula cha matanga, hasalimiki na atakuwa ni mwenye kupata dhambi kutokana na chakula hicho
Isipokuwa ikiwa chakula hicho kinatokana na mali za watu wengine wa mbali
Wallahu Aalam
Ustadh Shaaban Bin Salim Al-Battashi
Zanzibar
No comments:
Post a Comment