Headlines News :
KARIBU ZANZIBAR YETU BLOG, KWA HABARI MOTO MOTO KUTOKA JIKONI USIKOSE KUTUFUATILIA...ZANZIBAR MEDIA GROUP TUNAIWAKILISHA ZANZIBAR...
Home » » Je mtu akifa inafaa baada ya siku tatu kukusanyika na kumuombea Dua?

Je mtu akifa inafaa baada ya siku tatu kukusanyika na kumuombea Dua?

Je mtu akifa inafaa baada ya siku tatu kukusanyika na kumuombea dua?

Jawabu kutoka kwa Sheikh Shaaban Bin Salim Al-Battashi

Muisilaamu baada ya kufa kwake, anatakiwa kufanyiwa haki zake maalumu kisheria.


Na miongini mwa haki zake ni :

 Kulipwa madeni yake kutokana na asili ya mali yake
Kukafiniwa sanda
Kusaliwa
Kuzikwa
Kuombewa dua

Katika kuombewa dua hakuna muda maalumu ambao umewekwa kisheria kuwa ndio muda wa kumuombea maiti

 Wala hakuna Sunna yoyote ya kukusanyika watu na kumuombea dua maiti
 Mtume S.A.W alikuwa akiwaambia maswahaba r.a  baada ya kuzika maneno yafuatayo

"Muombeeni msamaha ndugu yenu, kwa hakika yeye hivi sasa ataulizwa"

Amma kukusanyika watu siku ya tatu, au arobaini, au mmwezi wa Rajabu, kwa ajili ya kuwaombea dua maiti, hili jambo halipo hatika sunna ya Mtume s.a.w, wala  yoyote katika maswahaba R.A

Bali hili jambo ni uzushi katika dini

Na wala hakuna thawabu kwa mwenye kualika watu kufanya matanga katika msiba, na mwenye kula chakula cha matanga, hasalimiki na atakuwa ni mwenye kupata dhambi kutokana na chakula hicho

Isipokuwa ikiwa chakula hicho kinatokana na mali za watu wengine wa mbali

Wallahu Aalam

Ustadh Shaaban Bin Salim Al-Battashi
Zanzibar 


















Share this article :

No comments:

Post a Comment

 
Support : Zanzibar Media Group
Copyright © 2020. Zanzibar Yetu - All Rights Reserved