ZAIDI ya watoto 30,000
wenye umri wa miezi 6 hadi miaka 5 wa wilaya ya Magharibi ‘A’ na ‘B’
wanatarajiwa kupewa chanjo za vitamin ‘A’ na dawa za minyoo kwa kipindi cha
mwezi mmoja ili kuwakinga na maradhi mbalimbali katika kipindi cha ukuaji wao.
Akizindua utoaji wa
chanjo kwa watoto katika kituo cha afya Magogoni, Mkurugenzi wa Manispaa Magharibi
‘B’ Amour Ali, amesema watoto chini ya umri wa miaka mitano wamekuwa wakiathirika
na kupata maradhi ikiwemo shrua, pepopunda, kuharisha na kupooza kutoka na
ukosefu wa chanjo.
Alifahamisha kuwa
chanjo zina umuhimu mkubwa kwa watoto kwani husaidia katika makuaji yao iwapo
watapata lishe pamoja na matone ya vitamin A hali itakayosaidia kustawisha afya
zao.
Daktari dhamana
wilaya ya Magharibi, Dk. Rahma Maisara, na Mtaalamu wa afya na lishe kutoka UNICEF,
Shemsa Mselem, walisema watoto walio
chini ya umri wa miaka mitano wamekua wakipoteza maisha kutokana na ukosefu wa
chanjo kutokana na upungufu wa damu unaosababishwa na ukosefu wa vitamin.
Nao wananchi
waliopatiwa huduma hiyo waliunga mkono jitihada za serikali za kuwapatia chanjo
watoto kwani zinasaidia kuwakinga na maradhi watoto wao jambo ambalo hapo awali
halikuwepo.
No comments:
Post a Comment